DRC RUTSURU

VYAKULA VYA PUNGUA BEI ENEO LINALO DHIBITIWA NA WAASI WA M23 KUTOKANA KWAMBA WAKULIMA HAWANA NAFASI YA KUSHAFIRISHA VYAKULA VYAO HADI ENEO ZINGINE KWA USALAMA.

FEBRUARI 26, 2024
Border
news image

wakaaji wa Rutsuru Mji wa Rutshuru na kiwanja ambao hawaku kimbia vita vya M23 na jeshi la serikali Pamoja na walio turoka kambi za wakimbizi kutokana na Maisha magumu wameanja kuwa na Maisha mazuri baada ya na mazao yao kuongezeka mashambani na kupungua bei kwa sasa . mfamo, gunia moja ya mahindi ambayo siku zilizo pita ilikuwa Iki uzwa kwa zaidi ya dola arbaini Mjini kiwanja kwa sasa ina uzwa kwa dola ishirini.

Mkaazi tulie zungumuza nae asema Kupungua kwa bei ya mahindi sokoni mijini Rutsuru imewafurahisha waliyo wengi wa eneo hilo japo wapo katika utawala wa waasi wa M23 wakiishi uhoga kila siku wakiogopa kushambuliwa ama kukamatwa na waasi wa M23 ama kupata matatizo wakati wa mapigano . Wakaaji wa kiwanja, Rutsuru na pempezoni mwa miji hiyo, wasema vizuizi kadhaa vilivyo kuwa vime wekwa na waasi wa M23 vimeondolewa na kodi za kutoka mashambani kupungua ila wakihitaji serikali kuhudumisha usalama na kuandaa uchaguzi eneo lao ili wawe na wabunge wao.

Wiki ilio pita M23 ilitangaza kuondoa masharti ya watu kutotembea usiku na wananchi wote eneo wanalo dhibiti kutembea bila shida japo kuna mapigano makali kati ya M23 na wazalendo wilayani masisi . Wakaazi wakienelea kutoa mwito na kulalamika serekali ya Drc kuwagomboa katika utumwa wanao pitia wakiwa wengi hawana uhuru wakujieleza wakisema wakaazi tulio zungumuza nao kwa njia ya simu.

NDIWELUVULA BIN MUTUME MTV NEWS Online